Saturday, October 8, 2011

HABARI KWA WAFUGAO KUCHA

Kufuga makucha ni kinyume na mafundisho ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) aliyenukuliwa katika hadithi mbali mbali akihimiza kuyakata.

Imepokelewa kutoka Bukhari na Muslim kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) amesema:

“Katika maumbile ni mambo matano; Akataja kukata makucha kuwa ni mojawapo ya mambo matano hayo.

Imepokelewa pia kutoka kwa Anas (RA) kuwa amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) ametuwekea muda wa kunyoa masharubu na kukata makucha na kusafisha nywele za kwapani na nywele zilizo juu ya sehemu za siri (visiachwe hivyo zaidi ya siku arubaini)

Kufuga makucha kunasababisha kukusanyika kwa uchafu mwingi chini yake na wadudu wanaoleta uchafu na kusahilisha kuwaeneza wadudu hao ndani ya vyakula na vinywaji.

Kufuga makucha pia kunaweza kuyazuwia maji ya udhu au ya tohara yasifikie sehemu ya ndani ya makucha hayo.

Kupaka rangi ya makucha pia kunasababisha maji yasiweze kuyafikia makucha na kwa ajili hiyo tohara haipatikani kwa njia sahihi.

Imepokelewa kutoka kwa Abu Ayub Al Ansari kuwa alikuja mtu kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) na kumuuliza juu ya habari za mbinguni. Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) alipomtizama mtu yule akaona kuwa ana makucha marefu, akamuambia: “Mmoja wenu anauliza juu ya habari za mbinguni wakati makucha yake ni marefu kama makucha ya ndege, anakusanya ndani yake janaba na uchafu.