SALAM ALAYKUM, Ndugu wote ;
Safari hii katika blog yetu ya www.kakasule.blogspot.com nakusudia kueleza japo kwa ufupi juu ya jaukaumu letu kama vijana na kama wanajamii wa kitanzania, kama inavyofahamika Tanzania ni nchi ya Amani na utulivu nawatu wake ni watu wa amani na utulivu. nayazungumza haya kwa aliyesahau akumbuke na anayejua azingatie.hivi karibuni kunatokea an kumetokea hali ambayo ss kama watanzania tunapaswa kuitizama kwa jicho la mara mbili Kumetokea mauaji ya wenzetu ambao bila shaka wanajulikana kuwa ni watanzania na wazalendo halisi wa nchi yao kwa munasaba kuwa eti walikuwa wanapigania haki, haki ya kumtafutia DIWANI FULANI cheo cha kuwa MEYA wa jiji la Arusha hivi huu ni uzalendo wa kufikia kuuwawa hivi kwa mungu twaweza kuja sema kuwa tulikuwa katika usahihi. Naomba nisieleweke vibaya kwa kuanza hivi bali pia sisemi kuwa hawakuwa katika usahihi bali twawajua Polisi na pia twajua nguvu za Dola nikimaanisha serikali, sasa najiuliza mara mbili walio katika haki ni walioua au kuuwawa kwa vile kila mmoja katoa ushahidi madhubuti kuwa alikuwa katika usahihi, sie tusiofungamana na upande wowote tunabaki kujiuliza haya.
Ok! labda kwa mtazamo wa wengi kuwa polisi wametumia nguvu iso halali kwa kulipinga jambo ila kwa taarifa walizotoa kwa mujibu wa uzito wa tunvyolichukulia jambo haikupaswa kufanyika vile nakusudia kwanza kwa waandamanaji pili kwa polisi, ila wajua siwalaumu wote kwa pamoja waswahili wanasema wapiganapo mafahari wawili ziumiazo nyasi ndiyo yaliyo wakuta wenzetu wa ARUSHA mafahari hapa nakusudia CHADEMA na SERIKALI/ Polisi wao waandamanaji na polisi wameponzwa na viongozi wao.
Kwanza waandamanaji wasingaliandamana kama sio wito wa viongozi wao an pia polisi wasingailiwapiga waaandamanaji kama sio tamko la amri ya viongozi wao. sasa, tutizame viongozi wapi waliowaponza waongozwa wao Je? ni wa CHADEMA ama Polisi?
CHADEMA wao dai lao la msingi ni kwa kura za umeya wa jiji la arusha ambalo wanataka walihodhi wao, wewe jiulize kwanza ungelikuwapo kwa akili yako juu ya hilo ungeliandamana mpaka kupambana na nguvu ya Polisi? Je kama ndio waujua hasa msingi wa dai hili upo kisheria na kuna mvutano au ukinzani wa kisheria, kama haja au haki ikiwepo huwa yaonekana kimsingi na hata asiye na haki hukiri mbona kwa swal hilo hilo la umeya Chadema wamepewa/ wamepata sehemu nyingine na pia hata kwa uwenyekiti wa halmashauri ambacho ni cheo sawa na umeya kwa ngazi hiyo wamepata katika sehemu nyingine? kama dai ni kuwa serikali inayoongozwa na chama cha CCM inawakandamiza kwaninbi iwakandamize ARUSHA tu kuna walakini, ila swala lenyewe lilivyokuwa ni kupishana jazba za kimaamuzi kwani wao CHADEMA hawajapiga kura na pia kuna taarifa za wao pia kumuingiza kiongozi diwani wa viti maalumu ambaye pia ana walakini na angeliweza kuleta tafrani nyingine. Arusha ni mji wa amani nahisi kuna watu wanataka kuufanya wa vurugu na kuiharibu hadhi yake mie ni mkazi wa huko sijaridhika na watu kuuwawa kwa sababu ya ladha ya Diwani fulani kutakiwa kuongezewa nguvu na cheo kuwa meya wa jiji.Chadema wangelikuwa na busara wasingelifikia pointi ya kuleta tafrani na polisi wangeliwatii na kubadili namna ya kupambana na viongozi wa serikali kwa mlango wa sheria, vyombo vya habari kufikisha ujumbe, na hata kupita ngazi zaidi siyo vurugu na maandamano kwani kuitazama mode waliyotumia naona sio sahihi wangapi bwana wameandamana Tanzania hii haya hata kwa histori yatuonesha failure na hata mafanikio yake sio yakaribu na yanagharimu muda na nguvu hata maisha, kama hivyo watu wamekufa, hivi Chadema ama CUF, mnafikiri kwakuandamana hii serikali yetu mtaishinda ingalikuwa hivyo wazee wetu wa EAST AFRICAN COMMUNITY wangelifanikiwa mapeema, kwani wameandamana sana. Hapa akili na hoja za msingi zitumike na si msingi wa hoja ujengwe hapana, nasema hapana kwa kuwa wenzetu hapa mmejeng msingi wa hoja na si hoja ya msingi kwani mnapoandamana na kufanya mikutano halafu serikali ikajidai haijasikia then mnafanyaje zaidi ya baadhi kuathirika sasa niulize je serikali jamii ya kimataifa na wengineo akina sisi tumesikia then what? samahani kama maneno yangu yatakuwa hayaingii akilini katika akili yako. Nafikiri hoja ya msingi ni hii ya mtayoifanya sasa badala ya maandamano na mikutano isiyo na mwisho, juweni nyie ni asilimia katika asilimia ndogo za watu wanaofuatilia na kuushinikiza muamala wa siasa na serikali katika nchi yetu, sasa nimesikia Dodom anao wanataka kuandamana sasa sijajua wale askari wa serikali watawafumbia macho, hii jamani mie naiona kama vurugu.
Msimamo wangu; nawashauri CHADEMA wakaechini wapunguze jazba, watatumia nguvu nyingi wenzao wameshika mpini wao makali watakatwa watafute mbinu mbadala za nje badala ya kuushikilia upande wa makali wenzao wakiuvuta zitabaki DAMU mikononi mwao. JAMBO la msingi watafute namna nyingine na mie sidhani kuwa viongozi wote wale kina Dk nani na mheshimiwa nani sijui ? kuwa hawana njia safi na mbadala ambayo haitawagharimu wafuasi wao.Jamani wewe mfuasi angalia maslahi yako nchi hii bwana wenye haki wachache wenye fursa pia wachache utapoteza mda wako bure, kwa mfano wewe mtu wa Dodoma meya wa Arusha akiwa meya takusaidia nini kwanza hivi watu wanajua hata hizo function za umeya au ushabiki tu? ok tujaalie tunajua wewe meya wa mkoa wako amekusaidia nini? najua kuna wataoniaona mzembe kwa kuuliza maswali kama haya ila nataka tujaribu kupima mimi naimani hata kama tukimpa meya wa Arusha awe CHADEMA point inabaki palepale kuwa Tatizo la Tanzania ni mfumo sio watu, kwani alipokuwa meya ni wa CCM tulidhurika nini na kaija mwingine atafanya kazi na serikali ipi? Jibu ni ile ile ambayo mnaiona ni mbaya je Niulize inamaana serikalini watumishi woote ni wabaya na kama sio nini kibaya kwa sababu serikali sio Raisi pekeyake bali Raisi ni sehemu. Jua hata tukiweka chama gani watanzania ni walewale kama huamini amini hili TATIZO NI MFUMO na sio vinginevyo kwani wewe huwaoni viongozi wa chadema wameongezeka serikalini kwa maaana ya chombo husika cha maamuzi katika nchi nakusudia Bunge sasa mpaka sasa wamejipanga vipi kuleta hayo wanayodai mabadiliko mie naona wanakimbilia maslahi yao tu hamna lolote. huu mie ndio msimamo na mtazamo wangu jamani usijenge chuki.
No comments:
Post a Comment